pmbet

ALEXIS SANCHEZ: Kutoka kuwa muosha magari makaburini hadi mwanasoka tajiri

Eric Buyanza

March 27, 2024
Share :

Alexis Sanchez alizaliwa tarehe 19 Desemba 1988 huko Tocopilla, Chile. Baada ya kuzaliwa, baba yake aliwatelekeza akimuacha na mama yake Martina Sanchez ambaye aliendesha maisha kwa kusagula biashara ndogo ndogo.
 

Katika kuhangaika na maisha ili apate riziki ya kulisha watoto wake, Martina ilimbidi aombe kazi ya kuparua samaki lakini hela hiyo haikutosha kutunza watoto wake watatu.
 

Katika hali ya kumsaidia Dada yake, ilimbidi mjomba wa Alexis amchukue dogo na kwenda kuishi nae na ndipo kwa msaada wa marafiki zake akafanikiwa kumuunga Dogo (Alexis) kwenye shule ya soka ya vijana wadogo iitwayo Arauco’s youth school.
 

Hata hivyo kutokana na ugumu maisha ilifika wakati mjomba alikosa hela ya kulipa ada ya shule, jambo lililomlazimu Alexis kutafuta kibarua.
 

Alexis ambaye kwa jina la utani utotoni aliitwa “El Nino Maravilla" (Mtoto wa ajabu) alipata kazi kuosha ya magari kwenye geti la kuingia makaburi ya jiji alilokuwa akiishi na pia alikuwa akiburudisha watu mitaani kwa kucheza sarakasi, na kickboxing (alilipwa kupigana na watoto wenzake) ili kujiingizia kipato.
 

Mwaka 2005 alipata nafasi ya kujiunga na klabu ya Cobreloa ya Chile ambapo uchezaji wake ulivutia wengi na kunyakuliwa na klabu ya Udinese ya Serie A.

Yaliyofuata baada ya hapo ni historia.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet