pmbet

Ali Kamwe yupo fresh

Sisti Herman

February 25, 2024
Share :

Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa Afisa habari na mawaasiliano wa klabu hiyo anaendelea vizuri baada ya kupata changamoto muda mchache kabla ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya CR Belouidad kumalizika huku Yanga wakishinda magoli 4-0 na kufuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa.

 

Kupitia ukurasa rasmi wa klabu ya Yanga zimechapishwa picha zikionyesha baadhi ya wachezaji pamoja na viongozi wa klabu hiyo wakiwa hospitalini kumjulia hali Ali Kamwe aliyezimia muda mchache kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika waliocheza dhidi ya CR Belouizdad kuisha huku wakisema anaendelea vizuri.

Katika picha hizo wameambatanisha ujumbe usemao " wananchi Ofisa habari wetu Ali Kamwe alipata changamoto dakika chache kabla ya mchezo wetu kuisha na kukimbizwa hospitali ya Agha Khan kupata matibabu na sasa anaendelea vizuri na yupo salama salmin".

Kamwe alikumbana na hali ya kuzimia wakati akishangilia ushindi wa mabao 4-0 waliyoyapata katika mchezo wa tano wa hatua ya makundi CAFCL dhidi ya CR Belouizdad uliochezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jana Februari 24, 2024 na kuwafanya kufuzu katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet