Ali Kiba aitaka jamii kuwasaidia watoto wenye uhitaji
Eric Buyanza
April 1, 2024
Share :
Nyota wa Bongo fleva na Bosi wa Crown FM 92.1, Ali Kiba ameitaka jamii kujenga tabia ya kuwasaidia watoto wenye uhitaji maalumu pindi mwenyezi Mungu anapowapa riziki ya kutosha.
Hayo ameyasema jana katika Iftar, iliyoandaliwa na kituo cha kulea watoto wenye uhitaji maalum (Mwandaliwa Orphanage Centre), kilichopo Mbweni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kufuturu, Ali Kiba amesema kuwasaidia watu wenye uhitaji maalum ni jambo la baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu.
Hata hivyo amesema, si vyema anapomsaidia mtu kijitangaza mara kwa mara kwa sababu vitu vya imani ninakwenda kwa imani.
“Mimi nilikuwa nakuja hapa kama mgeni mwalikwa lakini kwa sasa ni mwenyeji, huwa nakuja mara kwa mara lakini hakuna mtu anayejua, hivyo naiomba jamii kujenga tabia ya kuwasaidia watu hawa ili kupata baraka kwa Mwenyezi Mungu,” amesema Ali Kiba.