Alikosa Kombe la CAFCC Akiwa na Simba atalipata akiwa na USMA?.
Joyce Shedrack
April 20, 2026
Share :
Beki wa zamani wa Simba raia wa Cameroon Che Malone Fondoh ameandika historia ya kufuzu fainali ya Kombe la shirikisho misimu miwili mfululizo fbaada ya siku ya jana kutinga fainali ya michuano hiyo akiwa na klabu yake ya USM Alger ya nchini Algeria.

Hii inakuwa fainali ya pili mfululizo kutokana na msimu uliopita (2024/25) kuwa sehemu ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kilichofika hatua hiyo licha ya kutofanikiwa kutwaa kombe hilo mbele ya RS Berkane.
USM Alger ambayo imeiondosha Olympic de Safi kwenye michuno hiyo itacheza na Zamaleck ya Misri katika mchezo wa fainali.
Je Che Malone safari hii atafanikiwa kubeba ubingwa wa michuano ya Afrika kwa mara ya kwanza?.





