pmbet

Aliou Cisse hajalipwa Miezi 8 Libya

Sisti Herman

March 5, 2026
Share :

 

Shirikisho la Soka la Libya (LFF) limetoa tamko la kushtua likikiri kuwa limeshindwa kumlipa kocha mkuu wa timu ya taifa, Aliou Cissé, mshahara wake kwa kipindi cha miezi minane iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, ucheleweshaji huo unatokana na ukosefu wa fedha za kutosha ndani ya shirikisho hilo. 

Ukweli huu umeibua hofu juu ya mustakabali wa benchi la ufundi la timu hiyo, huku kocha huyo wa zamani wa Senegal akiendelea kuinoa "Mediterranean Knights" licha ya kukaa muda mrefu bila kupokea stahiki zake za kimkataba.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet