Alisimama kidete na mwanae Ronaldo, sasa anafanya kwa mjukuu
Eric Buyanza
November 14, 2026
Share :

Wakati mtoto wa Ronaldo (Cristiano Ronaldo Jr.) alipoingia uwanjani kwa mara ya kwanza kuichezea timu ya Ureno ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 (U-17), kamera za luninga zilielekezwa kwenye moja ya kona za majukwaa ya uwanja huo.
Kwenye kona hiyo anaonekana Bibi yake, Maria Dolores dos Santos Aveiro, akiwa ameketi anamuangalia mjukuu wake huku akiwa na tabasamu kubwa usoni.Ni hakika kabisa Bibi Maria hakuweza kukosa tukio hilo muhimu katika maisha yake.
Itakumbukwa Maria Dolores alikuwa bega kwa bega na mwanae Cristiano Ronaldo, na ndiye aliyekuwa nguzo kuu iliyopigania ndoto ya Ronaldo tangu akiwa mdogo huko kwenye mji wa Madeira nchini Ureno, licha ya maisha ya umaskini mkubwa kipindi hicho....na sasa anafanya vivyo hivyo kwa mjukuu wake.





