Aliyebaka wasichana wawili kwa zamu dukani aenda jela miaka 60
Eric Buyanza
February 29, 2024
Share :
Mahakama ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara hapa imemhukumu kifungo cha miaka 60 jela, mkazi wa Kijiji cha Mandi, Jeremia Lorri (45) baada ya kupatikana na hatia ya kuwabaka wasichana wawili kwa zamu.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Victor Kimario, alisema mahakama yake imemtia hatiani katika makosa mawili ya ubakaji.
Hakimu Kimario alisema kuwa siku ya tukio hilo, mshtakiwa huyo aliamua kujifungia dukani kwa mmoja wa wasichana hao na kuanza kuwabaka kwa zamu.