pmbet

Aliyeiba mtoto wa miezi 10 adakwa na Polisi

Sisti Herman

February 25, 2024
Share :

Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam wamemkamata Mariam Fransisco Renatus (22) kwa tuhuma za kumuiba Mtoto mwenye umri wa miezi 10 aitwaye Miracle Ayoub, eneo la Gongo la Mboto, Dar es salaam na kwenda nae hadi Kijiji cha Bugalama Mkoani Geita.

Kamanda wa Polindi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne amesema “Awali Jeshi la Polisi lilipokea taarifa za kuibwa kwa Mtoto huyo tarehe 06 Februari, 2024 majira ya saa moja usiku kutoka kwa Mama wa Mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Victoria Charles (34) Mkazi wa Gongo la Mboto, Mwizi huyo alijifanya Msaidizi wa kazi na baadaye kupata fursa ya kumuiba Mtoto huyo”

“Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa Mtuhumiwa alimuiba Mtoto huyo kwa lengo
la kuwaridhisha Familia ya Wakwe zake baada ya kuwadanganya kuwa alijifungua Mtoto tangu
mwezi wa Mei, 2023 baada ya kuwa na mahusiano na Kijana wao”

“Mtoto amepatikana akiwa na afya njema na Mtuhumiwa atafikisha haraka iwezekanavyo Mahakamani ili kijibu tuhuma zinazomkabili, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa Watu kuwa makini na Vijana wa kike wanaojifanya wanatafuta kazi za ndani na baadae kuweza kuwaibia”

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet