Aliyeishi na mwili wa mume wake akisubiri afufuke akamatwa
Eric Buyanza
April 27, 2024
Share :
Huko Kajiado nchini Kenya mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 58 anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kukutwa akiwa na mwili wa marehemu mume wake uliokuwa umeharibika vibaya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyorushwa na televisheni ya Citzen ya nchini humo, mwanamke huyo alikuwa ameuficha mwili wa mumewe kwenye nyumba iliyopo kwenye shamba lao eneo la Kitengela.
Inaelezwa kuwa wenyeji wa eneo hilo walivumilia kwa muda mrefu harufu kali iliyokuwa ikitoka kwenye nyumba hiyo, ndipo walipoamua kulijulisha jeshi la polisi ambao walivamia eneo hilo na kukuta mwili huo ukiwa umeharibika vibaya.
Baada ya kukamatwa mwanamke huyo kwanza alifikishwa Hospitali kwa ajili ya kupimwa akili.