pmbet

Aliyejeruhiwa kwa risasi 6 Kenya, bado anataka maandamano

Eric Buyanza

July 2, 2024
Share :

Kijana yatima wa miaka 18, Frank Okoth ni miongoni mwa Wakenya ambao wanadaiwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya kupinga Muswada wa Fedha wa 2024. 

Okoth, alipigwa risasi sita baada ya kundi la waandamanaji kuvamia Jengo la Bunge. 

Awali, ilidhaniwa kuwa Okoth, ambaye alipigwa risasi kifuani na tumboni alikufa kwa sababu ya majeraha aliyopata, lakini ripoti ya Citizen TV inaonyesha kuwa alinusurika. 

Okoth, ambaye sasa anauguza majeraha ya risasi nyumbani baada ya kuruhusiwa kutoka Hospitali, alisema ataendelea kuunga mkono maandamano dhidi ya serikali. 

Akiongea akiwa kitandani, Okoth alisema ingawa hawezi kutembea, ataunga mkono maandamano hayo hadi masuala yanayohusu vijana yatatuliwe. 

"Kabla ya maandamano nilikuwa nimeenda kutafuta kazi lakini sikufanikiwa, hivyo nilienda kufanya maandamano. Tunapaswa kuendelea kuandamana hadi tupate haki," Okoth alisema. 
TUKO

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet