Aliyekaa miaka 17 jela kimakosa, alipwa fidia ya shilingi Bilioni 2.6
Eric Buyanza
June 29, 2024
Share :
Mwaka 1999, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Richard Anthony Jones alihukumiwa kimakosa kifungo cha miaka 19 jela kwa kosa la wizi huko Kansas nchini Marekani.
Hata hivyo miaka 17 baadae akiwa gerezani anatumikia kifungo, ikabainika kuwa alifungwa kimakosa baada ya kufananishwa na mtu mwingine anayefanana nae ambaye ndiye mhalifu halisi.
Bwana Richard Jones alikuja kuachiwa huru Juni 7, mwaka 2017 na kulipwa fidia ya Dollar milioni moja (sawa na shilingi Bilioni 2.6 za kitanzania)