Aliyekuwa CHADEMA apewa 'Thank You' na wajumbe wa CCM.
Joyce Shedrack
August 5, 2025
Share :
Aliyekuwa Mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na baadae kutimkia Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku akisema alikuwa Chadema kwa mkopo Esther Bulaya ameshindwa kuongoza katika kura za maoni za kugombea nafasi ya Ubunge wa Bunda Mjini kupitia tiketi CCM.
Robert Maboto ambaye alikuwa mbunge wa wa Jimbo hilo ameibuka kinara baada ya kupata kura 2,545 huku Bulaya akipata kura 625.