Aliyekuwa kipa wa Simba afariki
Eric Buyanza
December 5, 2023
Share :
Klabu ya Simba kupitia taarifa kwa umma iliyochapishwa kwenye mitandao yao ya kijamii, inasikitika kupokea taarifa za kifo cha aliyekuwa kipa wao wa zamani Suleiman Ally Mussa kilichotokea visiwani Zanzibar baada ya kuanguka ghafla uwanjani wakati akifundisha timu yake ya Mchanga mdogo.
Simba inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huo.