Aliyembagua Rashford kwenda jela miezi 15
Sisti Herman
March 6, 2026
Share :

Shabiki wa klabu ya Real Oviedo ya nchini Hispania anakabiliwa na adhabu kali ya kisheria baada ya kuripotiwa kumtolea maneno ya kibaguzi mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford.
Mamlaka za kisheria zimechukua hatua kuhusu shauri hilo, na mtu huyo amehukumiwa kifungo cha hadi miezi 15 jelakwa kupatikana na hatia.
Hatua hii inaonyesha kuongezeka kwa msisitizo wa "kutovumilia kabisa" (zero-tolerance) unaochukuliwa na mamlaka za soka barani Ulaya pamoja na mifumo ya kisheria dhidi ya lugha za chuki na ubaguzi wa rangi michezoni.





