Aliyemtisha mwenzake kwa bastola, apigwa risasi na kufa
Eric Buyanza
July 20, 2024
Share :
Dereva mmoja mwenye hasira huko Indianapolis nchini Marekani alishuka kwenye gari yake akiwa na bunduki ili kwenda kumtisha dereva wa mbele yake aliyekuwa akizingua barabarani.
Hata hivyo baada ya kufika kwenye gari hiyo akiongea kwa hasira huku akimuonyeshea dereva mwenzake silaha akitumia mkono wake wa kulia, ghafla zilisikika risasi kadhaa zilizofyatuliwa kutoka ndani ya gari hiyo (pickup nyeupe) na jamaa aliyekwenda kumtisha mwenzake kudondoka chini na kufariki hapohapo.
Dereva aliyefyatua risasi kutoka kwenye pickup nyeupe alikamatwa na polisi lakini baadaye aliachiliwa baada ya wachunguzi kugundua kuwa huenda alifyatua risasi hizo kwa ajili ya kujilinda.