Aliyesajiliwa kwa Bilioni 200 Barcelona haonyeshi kiwango kombe la dunia
Eric Buyanza
June 24, 2026
Share :

Anthony Gordon yuko chini ya shinikizo la kutetea nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha England kabla ya mechi ya mwisho ya Kundi L dhidi ya Panama kwenye Kombe la Dunia Jumamosi.
Huo ni mtazamo wa wakongwe Gary Neville na Roy Keane, ambao wanaamini kwamba mshambuliaji huyo wa zamani wa Newcastle United yuko hatarini kuachwa kufuatia uchezaji mwingine mbaya wakati wa sare tasa ya England dhidi ya Ghana Jumatano.
Gordon mwenye umri wa miaka 25, ambaye hivi karibuni amejiunga na Barcelona akitokea Newcastle kwa dau la paundi milioni 71 sawa na shilingi bilioni 248.5 za Tanzania, hajafunga wala kutoa pasi kwenye mechi mbili za makundi za England.
Jambo hilo huenda likamfanya mwalimu kumuanzisha Marcus Rashford kwenye nafasi yake kwenye mchezo wa mwisho wa kundi dhidi ya Panama wikendi hii.
Rashford, 28, ambaye amekuwa akihusishwa na uhamisho wa pauni milioni 40 kwenda Newcastle majira ya joto, alifunga mara 14 na kutoa asisti 14 katika mechi 47 alizocheza kwa mkopo Barcelona msimu uliopita.





