Aliyetambulishwa na Simba Afrika atikisa ligi kuu ya Morocco.
Joyce Shedrack
April 13, 2026
Share :
Kocha wa zamani wa Simba Pablo Franco Martin ameendelea kuonesha ubora wake ligi kuu ya Morocco akiifundisha timu ya Maghreb de Fès baada ya usiku wa jana kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Wydad AC na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi.

Baada ya ushindi huo, Maghreb de Fès sasa wanashika nafasi ya kwanza wakiwa wamekusanya alama 31 baada ya mechi 15 huku Wydad Casablanca wakishuka hadi nafasi ya tatu wakiwa na alama 30, sawa na AS FAR ambao wamecheza mechi moja pungufu.
Pablo Franco amekiongoza kikosi hicho katika michezo 15 ya ligi pasipo kupoteza mchezo hata mmoja huku akitoa sare michezo 7 pekee.
Ikumbukwe kocha huyo timu yake ya kwanza kuifundisha barani Afrika ilikuwa ni klabu ya Simba mwaka 2021 alipojiunga nayo akitokea klabu ya Al Qadsia ya Nchini Kuwait.





