pmbet

Aliyeteka mtoto na kudai apewe milioni 1.5 akamatwa

Eric Buyanza

January 26, 2024
Share :

Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 3 na miezi 8 aliyetekwa na mtu asiyejulikana na kudai alipwe shilingi Milioni 1.5 ili amuachie huru ameokolewa na Jeshi la Polisi Mkoani Tanga.
 

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Almachius Mchunguzi ambapo alizungumzia tukio hilo ambalo lilileta sitofahamu kwa wananchi wa maeneo hayo.
 

Akieleza namna walivyomuokoa mtoto huyo,Kamanda Mchunguzi alisema Jan 23 mwaka huu saa kumi jioni Jeshi hilo kupitia vyanzo vyake lilipokea taarifa ya tukio hilo la kutekwa kwa mtoto huyo katika Mji Mpya wilayani Korogwe ambapo mtoto huyo alipatwa na janga hilo wakati akitokea kucheza katika nyumba ya jirani.
 

Aidha alisema kufuatia jitihada za Jeshi la Polisi Jan 25 nyakati za mchana katika kitongoji cha Sagama 'A' Kijiji cha Kwamkono Tarafa ya Sindeni wilayani Handeni Jeshi hilo lilifanya msako na kufanikiwa kumtia mbaroni Ramadhani Adinai Mbano (21) mkazi wa Manundu Korogwe akiwa na mtoto huyo.
 

Kamanda huyo alisema taratibu nyingine za kisheria zinakamilishwa ili mtuhumiwa huyo aweze kufikishwa Mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake huku mtoto akipelekwa kwa wataalamu wa afya kwa uchunguzi na taratibu za kumrejesha kwa mama yake zikifanyika

Kamanda Mchunguzi ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawalinda watoto wao kwa karibu ili kuwaepusha na vitendo vya watu wenye nia ovu kama vile utekaji,ubakaji na ulawiti kutokupata nafasi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet