pmbet

Almasi kutoka Saudia zamponza Rais, afunguliwa mashtaka

Eric Buyanza

July 5, 2024
Share :

Polisi wa Brazil wamemfungulia mashtaka Rais wa zamani wa nchi hiyo, Jair Bolsonaro kwa utakatishaji wa fedha na uhalifu kuhusiana na almasi ambazo hakuzitangaza.
 

Wakati akiwa madarakani, serikali ya Saudia ilimpa Bolsonaro na mkewe vito vya thamani ya dola milioni 3.2 ikiwa ni pamoja na mkufu wa almasi, pete na saa za kifahari.
 

Polisi walisema mwezi Agosti kwamba Bolsonaro alipokea pesa taslimu kutokana na mauzo aliyofanya karibia dola 70,000 kwa saa mbili za kifahari alizopokea kama zawadi kutoka Saudi Arabia.
 

Brazil inahitaji raia wake wanaowasili kwa ndege kutoka nje ya nchi kuweka wazi bidhaa walizoingia nazo kama zitakuwa zimezidi thamani ya Dola za Marekani 1,000, na ikiwa zimezidi thamani hiyo wanatakiwa walipie kodi inayolingana na asilimia 50 ya thamani hiyo.
 

Hata hivyo Rais huyo angeweza kusamehewa kodi kama angeziweka wazi kwasababu ingeonekana kuwa ni zawadi kutoka taifa moja kwenda lingine na hivyo zingeorodheshwa kama mali za taasisi ya URais, lakini hakutaka kutangaza na kuziingiza kinyemela bila mamlaka za serikali kuwa na taarifa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet