Alonso alivyofikisha 'Unbeaten' 46 kwa magoli ya dakika za 'jioooni'
Sisti Herman
April 28, 2024
Share :
Baada ya sare ya 2-2 dhidi ya Stuttgart kwenye ligi kuu nchini Ujerumani(Bundesliga), klabu ya Bayer Leverkusen sasa imefikisha michezo 46 bila kupoteza msimu huu kwenye mashindano yote inayoshiriki ambapo hadi sasa wameshatwaa Ubingwa Bundesliga huku wakiwa kwenye nusu fainali 2. kombe la Europa na kombe la ligi Ujerumani DFB Pokal.
Stori kubwa kwasasa kwenye 'UNBEATEN' ya Leverkusen ni namna wanavyolinda matokeo yao ya kutoruhusu kufungwa kwani kwa siku za karibuni wameshinda michezo mingi kwa magoli ya dakika za mwisho 'Jioooni' ili kuendelea kulinda heshima yao hiyo.
Hizi ni mechi ambazo Leverkusen wameshinda dakika za jioni;
90'+4 v Bayern
90'+4 v Qarabag
90'+4 v Augsburg
90'+1 v Leipzig
90'+1 v Stuttgart
90'+2 v Qarabag
90'+3 & +7 v Qarabag
90'+1 v Hoffenheim
90'+7 v Dortmund
90'+7 v Stuttgart
Hadi sasa Leverkusen msimu huu wameshacheza mechi 46 bila kufungwa wakiwa na sare 6 na ushindi mara 40.
Je nani anaweza kuwazuia Leverkusen msimu huu?