pmbet

Alonso humwambii kitu kwa Palmer

Sisti Herman

July 16, 2025
Share :

 

Kocha wa klabu ya Real Madrid, Xabi Alonso, anaripotiwa kuwa ni shabiki mkubwa wa kiungo mshambuliaji wa Chelsea, Cole Palmer, huku vigogo hao wa soka la Hispania wakidaiwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu maendeleo ya mchezaji huyo.

Kwa mujibu wa chanzo kutoka E-Notícies, Real Madrid wameonesha nia ya dhati ya kumtaka Palmer, ambaye ameonesha kiwango bora akiwa na Chelsea msimu uliopita.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa Chelsea haiko tayari hata kuzungumza juu ya uwezekano wa kumuuza nyota huyo, ikisisitiza kuwa Palmer ni mchezaji muhimu kwenye mipango ya klabu hiyo kwa sasa na siku zijazo.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet