pmbet

Amanda awa mwanamke wa kwanza Mnigeria kuwa Brigedia Jenerali kwenye jeshi la Marekani

Eric Buyanza

February 1, 2025
Share :

Amanda Azubuike, Ofisa wa kijeshi mweusi mwenye asili ya Nigeria, ameweka historia kuwa mwanamke wa kwanza wa Nigeria kuwa Brigedia Jenerali katika Jeshi la Marekani.

Azubuike mwenye umri wa miaka 57 ana asili ya Nigeria na Zimbabwe. Baba yake, alihamia Uingereza akiwa na umri mdogo kusomea sheria, akakutana na mama yake, mwanafunzi wa uuguzi kutoka Zimbabwe na kufunga ndoa. 

Hata hivyo walitalikiana na mama yake akahamia Marekani akiwa na Amanda pamoja na dada yake, ambapo Amanda hatimaye akazawadiwa uraia wa Marekani mwaka 1989.

Alipata digrii yake ya kwanza ya Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Central Arkansas mwaka 1993 na kujiunga na Jeshi mwaka 1994 kama rubani wa ndege baada ya kuhitimu kozi ya usafiri wa anga. Na hapo ndipo safari yake ya mafanikio kwenye jeshi la Marekani ilipoanzia.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet