Amber Rose akasirishwa na wanaomchukia Trump
Eric Buyanza
May 27, 2024
Share :
Mwamamitindo maarufu na aliyewahi kuwa mpenzi wa Rapa Kanye West, Amber Rose kwa mara nyingine ameibuka kumtetetea na kumuunga mkono mwanasisasa mtata aliyewahi kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump.
Wakati weusi wengi wa nchi hiyo wakimuona Donald Trump kama mbaguzi, mwanamitindo huyo aliyewahi kuwa mpenzi wa Rapa Kanye West, anasema baadhi ya wamarekani wamekuwa wakiaminishwa uongo na vyombo vya habari ili kumchukia Trump bila sababu za msingi.