pmbet

Amburuza mkewe mahakamani, kwa kumtoza pesa kila wakifanya tendo la ndoa

Eric Buyanza

June 6, 2024
Share :

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, huko nchini Zambia mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Aaron Kando mwenye umri wa miaka 53, ameshindwa kuvumilia unyanyasaji anaofanyiwa na kuamua kuweka wazi mbele ya Mahakama jinsi mke wake anavyomtoza (Kwacha 500) kila alipotaka kushiriki nae tendo la ndoa.

Aaron pia alisimulia mbele ya mahakama jinsi mkewe, Romance Shanzi, alivyoolewa kwa siri na mwanamume mwingine pale alipohamishwa kikazi Mkoani Muchinga.

Mbele ya Mahakama hiyo, Shanzi alikana kuolewa na mwanaume mwingine lakini alikiri kumtoza pesa mumewe kila alipotaka kulala naye.

Shanzi alisema alilazimika kumtoza pesa, kwasababu mume huyo hutumia pesa nyingi kununua makahaba huku akishindwa kuhudumia familia yake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet