pmbet

Amburuza mumewe Mahakamani, kisa uvivu wa kuoga!

Eric Buyanza

February 1, 2024
Share :

Hivi majuzi mwanamke mmoja wa Kituruki alifungua kesi mahakamani dhidi ya mumewe, akidai mwanaume huyo huwa anaoga kwa nadra sana, ananuka jasho, na mswaki huwa anapiga mara moja au mbili tu kwa wiki.
 

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la A.Y, aliomba talaka kutoka kwa mumewe na kuzitaja sababu za kuomba talaka kuwa ni kushindwa kuvumilia uchafu wa mwanaume huyo.
 

Wakili wa mlalamikaji aliiambia Mahakama ya Familia huko jijini Ankara kwamba mshtakiwa pia huwa anavaa nguo moja kwa siku 5 mfululizo bila kubadili.
 

Mashahidi ambao ni majirani walioitwa mahakamani hapo kuthibitisha madai hayo, wote walitoa taarifa za kuthibitisha hali ya uchafu ya jirani yao.
 

Hatimaye Mahakama ilikubali ombi la mwanamke huyo la talaka na pia kuamuru mume amlipe mke wake Lira 500,000 za Kituruki (sawa na milioni 42 za kitanzania) kama fidia kwa kuvumilia hali hiyo ya uchafu kwa muda wote walioishi pamoja.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet