pmbet

Amchoma jirani yake na mafuta ya moto, kisa kamuiga style ya nywele!

Eric Buyanza

January 31, 2024
Share :

Huko nchini Kenya limetokea tukio la kusikitisha baada ya mwanadada aliyetambulika kwa jina la Catherine Wanjiru kummwagia jirani yake mafuta ya moto.
 

Taarifa ya polisi nchini humo inasema Catherine alimmwagia usoni mafuta yaliyotoka jikoni Sherry Nyanchomba na kumsababishia majeraha makubwa.
 

Inadaiwa kuwa Januari 16 majira ya sita usiku Catherine alikutana na Sherry mbele ya mlango wa nyumba yao wanayoishi na alipoona jirani yake ametengeneza nywele kama zake alichukia na kumshutumu Sherry kwa kumuiga. Wawili hao, walikuwa na nywele zenye rangi zinazofanana.
 

Kwa hasira Catherine alikimbilia kwenye kijiwe cha mkaanga samaki aliyekuwa jirani na kubeba  mafuta na kummwagia mwenzake usoni hali iliyozua tafrani kubwa.
 

Sherry alikimbizwa hospitali kwa matibabu ambapo Catherine alifikishwa polisi na baadaye kufunguliwa kesi mahakamani.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet