pmbet

Amchoma moto mdogo wake kisa kula ndizi!

Eric Buyanza

January 6, 2024
Share :

Mtoto Rose Sagauli (7) mwanafunzi wa awali katika shule ya msingi Mji Mwema iliyopo Mtaa wa Mji Mwema Halmashauri ya Mji Njombe mkoani Njombe, amechomwa moto mikononi na kaka yake Zedekia Maguchi (18) mwanafunzi wa kidato cha tano kwa tuhuma za kula ndizi mbili..kwenye tukio lililotokea Januari 3.
 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Mji Mwema, Leonard Mkupi inadaiwa kuwa sababu ya mtoto huyo kuchomwa moto ni mara baada ya kuhisi njaa na kuingia ndani kuchukuwa ndizi mbili na kula.
 

“Kaka yake akamkamata na kumfunga mikono yote miwili akawasha jiko la kuni na kumchoma moto,” amesema Mkupi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet