pmbet

Ameandika Afande Sele: Uvccm wanakosa kwao ukomavu na uvumilivu wa kisiasa

Eric Buyanza

June 12, 2024
Share :

Wakati mkuu wa nchi mwenyewe Mh Rais Dr Samia,akionyesha ukomavu na uvumilivu mkubwa wa kisiasa kwa kufuata mfano wa Chura ,wa kutohangaishwa wala kuchukizwa na maneno ya wakosoaji wake,😩
 

Hawa vijana wa Uvccm ambao ndio viongozi wa taifa la kesho,wanatoa kauli zinazoonyesha kukosa ukomavu na uvumilivu wa kisiasa,katika taifa linalojipambanua kuheshimu demokrasia na Uhuru wa kutoa maoni 🗣️
 

Tukumbuke ni hivi juzi tu,kuna kiongozi wa Uvccm mkoani Kagera alitamka hadharani kuwa,watu wote wanaowakosoa viongozi wa chama na Serekali, watawapoteza kimyakimya na polisi isiwatafute,..Na sasa viongozi wengine wa Uvccm wanataka serekali ifunge mitandao kwasababu ya kukosa kwao ukomavu na uvumilivu wa kisiasa,ambavyo ni miongoni mwa vigezo muhimu kwa mwanasiasa yoyote duniani katika kujenga mustakabali mwema wa jamii yake🙏
 

Kwa akili za kawaida tu,unagundua kauli hizo hatari za hawa Uvccm ni sawa na kutangaza mfarakano ndani ya jamii au uasi wa kitaifa,kwasababu matokeo ya kuwaziba midomo watu wasitoe maoni yao ili kupunguza machungu yao,,huwa ni kuwalazimisha watu hao watafute "Plan B"ya kutoa hayo machungu yao,huku mara nyingi katika maeneo mengi,tumeshuhudia hiyo Plan B huwa sio maneno tena,bali ni vitendo,huku vitendo hivyo huwa havimuachi salama mtu yoyote ndani ya jamii hiyo.☠️
 

Hizi kauli hatarishi,za kizembe na kipuuzi kutoka kwa vijana hawa wa chama tawala,zitazamwe kama ishara ya hatari inayotukabili kama taifa,siku za baadae endapo vijana hawa wavivu wa kufikiri watashika nafasi kubwa za kiuongozi na maamuzi ya taifa hili.🇹🇿
 

Upuuzi wao mkubwa zaidi ni kuamini kuwa kila mtumiaji wa mitandao,anafuata "udaku" na "Ubuyu"tu,bila kujua wala kujali kuwa kuna maelfu ya watu hasa vijana wenzao wasiokua na konekshen za ajira za serekali kama wao wa kishua,,walioamua kujiajiri kupitia hiyo mitandao ya kijamii wanaotaka ifungiwe✊

Bora ukemee Mabaya na Usifie Mazuri.👍
Ni Mtazamo Tu😎

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet