pmbet

AMEANDIKA JEMEDARI SAID: "Kwanini naamini CPA Issa Masoud hajakosea"

Eric Buyanza

June 10, 2024
Share :

Kuna kitu kinanishangaza sana kutoka kwa mashabiki na wanachama Simba SC ni namna walivyo mafundi wa kugeuka geuka, kuna wakati walitaka viongozi wao watoke na waseme yanayoendelea mwenye klabu yao baada ya fununu kwamba mambo hayako sawa.
 

Leo viongozi wanatoka na kuja kusema yanayoendelea ndani kama walivyojitaji, wanageuka na kusema ooooh mbona hamkusema tangu mwanzo, mnasubiri mpaka ligi iishe na tajiri aombe wajumbe wa upande wake wajiuzulu ndo mnatoka kusema, nyinyi ni waongo.
 

Yani mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya Fedha ya Simba (CAG wa klabu) ambaye anashiriki kwenye vikao vikubwa, vidogo na nyeti, anakuambia hali halisi kama ulivyotaka kuisikia, halafu we hutaki ukiamini tajiri hakosei ila watu wanakula hela zake.
 

Binafsi naamini CPA Issa Masoud na wenzie walitumia busara kubwa kuyavumilia mambo na kujaribu kuyamaliza wakiwa ndani ili kujenga umoja, wanapoona mwekezaji hataki suluhu ya ndani anakuja nje kwa kupigia simu na kushinikiza “wajumbe wake” waondoke kwenye bodi, wana amua kuyaweka wazi ambayo mwekezaji hakutaka wayaongee ndani, kosa lao nini? Au umasikini umetupumbaza na kuamini tajiri hakosei?
 

Kuna suala la kwamba watu wanakula pesa za tajiri na kwamba tajiri anapata hasara. Sijaona mfanyabiashara huyo ambaye anaweza kuwa anatoa pesa kwa watu wanakula miaka 2 na bado anatoa mwaka 1 mwingine wazidi kuzila pesa zake, hii haiwezekani. Hapa panatafutwa pahala pakujifichia na kutaka kutokea tu. 

Sijaona mfanyabiashara ambaye anapata hasara kwenye baiashara miaka 5 na bado ameng’ang’ana na biashara hiyo hiyo kwa mbinu hizo hizo zinazompa hasara. Sikilizeni hoja chambueni kwa makini msiweke hisia mtaelewa.
 

NARUDI….,

BIN KAZUMARI MTIPA (The voice of the voiceless)

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet