Amfanyia upasuaji mtoto aliyemtoa tumboni na kumrudisha
Eric Buyanza
March 23, 2026
Share :

Katika hali ya kushangaza ambayo tunaweza kuiita ni mafanikio makubwa ya kitabibu, mwaka 2016 Daktari bingwa wa upasuaji wa watoto aliyezaliwa Nigeria, Dkt. Oluyinka Olutoye alifanikiwa kumfanyia upasuaji mtoto mchanga akiwa bado ndani ya tumbo la uzazi la mama yake.
Mtoto huyo aliyekuwa na wiki 23 alitolewa kwa uangalifu ili madaktari waweze kufanya upasuaji kutokana na hali iliyokuwa ikitishia maisha yake ambayo haingeweza kusubiri hadi azaliwe.
Baada ya upasuaji uliofanikiwa, mtoto alirudishwa ndani ya tumbo la mama ili aendelee kukua kwa usalama.
Miezi kadhaa baadaye, mtoto huyo alizaliwa akiwa na afya njema.
Kweli huu ni muujiza wa sayansi na maisha.





