pmbet

Amfyatulia risasi mke wake na kumuua mbele ya binti yao wa miaka 10

Eric Buyanza

March 21, 2024
Share :

Mwanaume mmoja huko Afrika Kusini amemuua mke wake kwa kumpiga risasi ya kichwa na kisha kujigeukia yeye na kujipiga risasi mbele ya macho ya binti yao wa miaka 10.

Kisa hicho kilitokea Saunders, Belvedere KwaZulu-Natal Jumatano ya Machi 20/2024 huku taarifa zikidai wakati tukio linatokea wawili hao walikuwa wametengana.

Inaelezwa kuwa jamaa huyo alifika eneo hilo akiwa na gari la ofisini kwake kwa ajili ya kuja kumchukua binti yake na ndipo ghafla ugomvi na majibizano yalipozuka, jamaa bila kuchelewa akachomoa bastola aliyokuwa nayo kiunoni na kumtandika mke wake kichwani na kisha kujitandika na yeye.

Hata hivyo jamaa huyo hakufariki lakini alijeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali akiwa katika hali mbaya.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet