Amina aenda jela miaka 7, kwa kukeketa mtoto wa Uingereza
Eric Buyanza
February 17, 2024
Share :
Mwanamke mmoja anayeishi nchini Uingereza aliyefahamika kwa jina la Amina Noor amehukumiwa kwenda jela miaka 7 kwa kusaidia kumpeleka mtoto wa Uingereza wa miaka 3 nchini Kenya kwa 'ngariba' kukeketwa.
Amina anayeishi Harrow, kaskazini-mashariki mwa London, alisafiri hadi Kenya mwaka 2006 akimsindikiza rafiki yake (mwanamke wa kikenya) kumpeleka mtoto wake aliyekuwa na umri wa miaka 3 wakati huo (mzaliwa wa uingereza) kwa ajili ya kukeketwa.
Amina aliiambia mahakama ya Old Bailey kwamba ukeketaji unafanywa kwa sababu za kitamaduni na ulikuwa utaratibu ambao hata yeye mwenyewe aliupitia alipokuwa mtoto.