Amini Usiamini, ni YEYE...Operation ya kurudisha UJANA, yawa gumzo
Eric Buyanza
June 4, 2024
Share :
Huko Instabul nchini Uturuki, kliniki moja ya kufanya 'Plastic Surgery' imekuwa gumzo duniani kote baada ya picha za mteja wao waliyemdumia kwa kumfanyia upasuaji wa kurudisha UJANA kufanikiwa kwa kiwango cha ajabu.
Kliniki hiyo inayofahamika kwa jina la Este Med, ilipost kwenye mtandao wa Instagram picha za mgonjwa wao za kabla na baada ya upasuaji, ambazo zilimuonesha mzee huyo akiwa kijana kabisa.
Mzee huyo aliyefahamika kwa jina la Michael picha zake zilifanya wengi wasiamini kuwa ni mtu yuleyule kutokana na mabadiliko makubwa waliyoyaona, mabadiliko ambayo hata wataalm wengine wa “Plastic Surgery' duniani yaliwashangaza.
Katika post yao ya Instagram, Este Med walidai kwamba Michael alipitia hatua kadhaa za upasuaji mpaka kufikia mabadiliko hayo ya kushangaza
Hatua hizo ni pamoja na kuinua nyama za uso, nyama za shingo, kurekebisha kope za chini, kuondolewa mafuta na upandikizwaji wa nywele.