pmbet

Ammwagia mumewe maji ya moto, kisa! Kamuota mwanamke mwingine

Eric Buyanza

July 13, 2024
Share :

Mwanamke mmoja huko nchini Bolivia alitiwa mbaroni kwa kosa kummwagia mume wake maji ya moto sehemu za siri akiwa usingizini kisa alimsikia wakiwa wamelala akimuota mwanamke mwingine.

Tukio hilo la kushangaza lilitokea katika jiji la La Paz ambapo inaelezwa baada ya mwanamke huyo kumsikia mumewe alipatwa na hasira, akaingia jikoni, kuchemsha maji na kisha akaingia chumbani na kummwagia mume wake sehemu za siri.

Mwanaume huyo alilazwa hospitali kwa siku kadhaa akitibiwa majeraha ya moto sehemu za siri, mkononi na sehemu ya mgongo.

Juan José Donaire, naibu mkurugenzi wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Uhalifu kwenye jiji la La Paz, alisema kuwa hii si mara ya kwanza kwa mwanamume huyo kufanyiwa ukatili na mkewe, kwani siku za nyuma mwanamke huyo aliwahi kummwagia pombe kali na kujaribu kumchoma moto.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet