pmbet

Amng'oa mke wake meno 3 kwa koleo, kisa shilingi 200

Eric Buyanza

July 10, 2024
Share :

Jeshi la Polisi mkoani Mara linamshikilia mkazi mmoja wa Kijiji cha Nyakatende wilayani Musoma, Musa Abdallah kwa tuhuma za kumn'goa meno matatu mke wake kwa kutumia ‘pliers/koleo’ kwa kile kinachoelezwa ni ugomvi wa Shilingi 200. 

Inadaiwa mtuhumiwa huyo ambaye ni mganga wa kienyeji alitenda ukatili huo baada ya mke wake huyo kutumia fedha hizo, zilizotokana na mauzo ya mahindi kununua mahitaji ya mtoto wao mdogo bila idhini yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salum Morcase, alithibitisha tukio hilo akisema mtuhumiwa huyo akisaidiana na mke wake mwingine ambaye bado hajatiwa nguvuni walimkamata mke mdogo wakamlaza chini na kisha mume wake akamn'goa meno matatu.

"Mtuhumiwa huyo akisaidiana na mke wake wa pili walimshika mama huyo na kumlaza chini huku wakiwa wamemshikilia ambapo kwa kutumia pliers aliweza kutenda ukatili huo na kumsababishia maumivu makali," alisema.

Kamanda Morcase alisema hata hivyo, baada ya kutenda ukatili huo mtuhumiwa huyo ambaye yuko mikononi mwa polisi alimfungia ndani ya nyumba hadi taarifa kutoka wasamaria wema zilipofika polisi. 
"Kwa sasa tunamshikilia kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi ili hatua sahihi zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kumfikisha mahakamani kutokana na makosa yanayomkabili ili sheria ichukue mkondo wake," alisema.

Picha zilizotumika sio halisi (hazihusiani na habari hii).

NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet