Amorim amtolea udenda beki tegemeo wa Benfica
Eric Buyanza
November 29, 2024
Share :
Usajili Kocha wa Manchester United, Ruben Amorim ameelekeza macho yake kwa beki wa kati tegemeo wa Benfica, Tomas Araujo ikiwa ni mikakati yake ya kuisuka vyema safu yake ya ulinzi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa na msimu mzuri na Amorim anaripotiwa kutenga dau la pauni milioni 50 wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa Januari 2025.
Araujo amekuwa mtu muhimu katika safu ya ulinzi ya Benfica, akishirikiana na Nicolas Otamendi.