Amri 10 za Mungu kubandikwa kwenye madarasa ya shule na vyuo
Eric Buyanza
June 20, 2024
Share :
Louisiana limekuwa jimbo la kwanza nchini Marekani kutumia sheria mpya iliyosainiwa Jumatano wiki hii na Gavana wa Republican, Jeff Landry, inayolazimisha kila darasa kwenye shule za umma kuanzia chekechea mpaka vyuo vikuu vinavyomilikiwa na serikali kuweka bango kubwa linalosomeka kiurahisi litakalozionesha 'Amri kumi za Mungu'.
"Ikiwa unataka kuheshimu utawala wa sheria, basi yakupasa uanze kutoka kwa mtoa sheria wa kwanza, ambaye ni Mussa aliyeshushiwa amri kutoka kwa Mungu,” alisema Gavana Landry.
Wapo walioipinga sheria hiyo wakihoji uhalali wake na kuapa kuipinga mahakamani.