Amri ya kutotoka nje yaanza kutekelezwa jijini Los Angeles
Eric Buyanza
June 11, 2025
Share :
Meya wa Los Angeles Karen Bass ametangaza amri ya kutotoka nje katika jiji Los Angeles kukomesha uharibifu unaofanyika.
Bass amesema amri ya kutotoka nje itatekelezwa kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi.
Mkuu wa polisi wa jiji hilo, Jim McDonnell, alisema amri ya kutotoka nje ni hatua muhimu ili kuokoa maisha na kulinda mali baada ya mfululizo wa machafuko yanayoongezeka katika jiji hilo.
Alisisitiza kuwa watu watakaovunja amri ya kutotoka nje watakamatwa.
Wakati huo huo, Jaji wa Marekani alizuia ombi la dharura kutoka kwa Gavana wa California la kutaka kuzuia kutumiwa kwa wanajeshi kwenye vurugu zilizoshuhudiwa katika mji wa Los Angeles.
Gavana Gavin Newsom ameitaja hatua hiyo kuwa kinyume na sheria.
Rais Donald Trump ametetea uamuzi wake wa kutuma majeshi kukabiliana na waandamanaji wanaopinga sera kali dhidi ya sera mpya za wahamiaji na kuapa kuwa kamwe hataruhusu mji wowote wa Marekani kuvamiwa na kutawaliwa na wageni.
BBC