pmbet

Amrouche kukta rufaa

Sisti Herman

January 21, 2024
Share :

Kwa mujibu wa Taarifa zinasema kuwa kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Adel Amrouche anajipanga kukata rufaa juu ya maamuzi ya kufungiwa yaliyotolewa na shirikisho la soka Afrika [CAF].

 

” Ninajiandaa kwenda kukata rufaa juu ya adhabu niliyopewa”.

 

“Mwanasheria wangu amenishauri nisizungumze na vyombo vya habari, kwahiyo siwezi kuzungumza sana kwasasa”.

 

“Lakini ni vipi naweza kufungiwa bila kupewa barua ya nidhamu au kusikia?, hii inawezaje kuwa sawa ? Haki iko vipi hapo ?”, Alisema kocha Adel Amrouche.

 

Adel amefungiwa kusimama kwenye benchi la ufundi kwa takribani miezi nane [8] kutokana na shutuma alizozito kwenda shirikisho la soka la Morocco.

Kwasasa Taifa Stars inaongozwa na makocha wake wasaidizi Juma Mgunda na Hemed Morocco kuelekea mchezo ujao wa hatua ya makundi dhidi ya Zambia na ule wa DR Congo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet