Amshambulia kwa kisu mama anayeiunga mkono Palestina na kumuua
Eric Buyanza
June 4, 2024
Share :
Mwanamume mmoja huko Afrika Kusini amefikishwa mahakamani Jumanne hii akishtakiwa kwa mauaji baada ya kumchoma kisu mama mmoja hadi kufa katika kitongoji cha Durban na kuwajeruhi mwanae na mumewe kwa sababu ya kuiunga mkono Palestina.
Mwanamke huyo alikufa papo hapo, ambapo mumewe na mtoto wake walichomwa visu mara kadhaa na kujeruhiwa vibaya.
Polisi imesema mwanaume aliyefanya uhalifu huo alikamatwa eneo la tukio akiwa na kisu chenye damu.