Amuibia mpenzi elfu 10 akabet, mkeka ukampa milioni 100
Eric Buyanza
March 31, 2026
Share :
#JeWajua Mwaka 2021, mwanamume mmoja huko nchini Nigeria aliripotiwa kumuibia kwa siri mpenzi wake 10,000 na akaitumia kubetia.
Cha kufurahisha ni kwamba mkeka wake uliitika na kumuingizia milioni 100 (pesa ya kinigeria).
Baada ya mpenzi kujua chanzo cha ushindi ule ilikuwa ni hela yake iliyokuwa imechukuliwa bila ridhaa, akamtaka mwanaume ampe mgao angalau wa milioni 40 jambo ambalo jamaa alikataa na kumpa milioni 5 pekee.






