Amuua kondakta wa daladala kisa shilingi 100!
Eric Buyanza
February 27, 2024
Share :
Kijana wa miaka 28 aliyefahamika kwa jina la Venance Ngonyani, mkazi wa mtaa wa Mahenge Manispaa ya Songea, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Ruvuma kwa kosa la kumchoma kisu na kumuua kondakta wa daladala aliyefahamika kwa jina la Hussein Anaf.
Inaelezwa kuwa siku ya tukio Venance alipanda daladala akiwa na shilingi 500 na kumpa konda (Hussein) wakati nauli halali ni shilingi 600, wakati Hussein alipokuwa akimsisitizia Venance aongeze 100 kulizuka malumbano baina yao ndipo Venance (mtuhumiwa) alipochomoa kisu na kumchoma Hussein shingoni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani Ruvuma, ACP Marco Chilya tukio hilo lilitokea Februari 25, 2024 majira ya saa 12 jioni katika stendi ya Mkuzo iliyopo kata ya Msamala wilayani Songea.