Amuua mkewe na kumhifadhi juu ya dari
Eric Buyanza
December 7, 2023
Share :
Mwanaume mmoja huko Kakamega nchini Kenya aliyetambulika kwa jina la Isaya, amefanya tendo la kikatili baada ya kumuua mke wake aliyekuwa akimsaliti na mwanaume mwingine na kisha kuuficha mwili wake juu ya dari, na yeye kufanya maamuzi ya kujiua kwa kujinyonga.
Ukatili huo kwa mujibu majirani umefanyika kutokana na wivu wa mapenzi, huku majirani hao wakishuhudia kusikia mara kwa mara wanandoa hao wakigombana kuhusu swala hilo la kusalitiana.
Taarifa hizo zinadodosa kuwa mume alistukia michezo ya mke wake baada ya kufuatilia simu yake ya mkononi, na baada ya kumbana sana mke huyo alikubali kuwa anamsaliti jamaa na mwanaume mwingine na huwa anamleta hapo nyumbani na kushiriki nae mapenzi kwenye kitanda chao mara kwa mara.