pmbet

Amuwekea binti yake kisu kwenye begi la shule kwa ajili ya ulinzi

Eric Buyanza

February 23, 2024
Share :

Staa mkongwe wa filamu za mapigano, Sylvester Stallone..ambaye wengine wanamkumbuka kwa jina la (ROCKY au RAMBO) kutokana na movie zake za zamani zilizowahi kutikisa dunia miaka ya nyuma, amegusa kurasa nyingi za vyombo vya habari baada ya mtoto wake wa kike kuelezea jambo ambalo limewashangaza wengi.
 

Ni hivii, mbabe huyo ambaye kwasasa amezeeka lakini bado akiendelea kufanya vizuri kwenye uigizaji, aliwahi kumuwekea kisu kwenye begi la shule binti yake aitwae Sistine wakati alipokuwa (darasa la nne) kama njia ya kujilinda na mtu yoyote atakayemzingua, sasa hivi binti huyo ana miaka 25.
 

Sylvester ambaye kwasasa ana umri wa miaka 77, ana mabinti watatu aliowazaa na mkewe Jennifer Flavin.

Inaelezwa kuwa mabinti hao wa Sylvester Stallone usiwachezee kabisa kwasababu baba yao tangu wakiwa wadogo amekuwa akiwafundisha mbinu za mapigano za kujihami na adui.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet