Ana mimba ya mtoto wa 20, asema ataendelea kuzaa mpaka mwili ukatae!
Eric Buyanza
February 2, 2024
Share :
Huko nchini Colombia mwanamke mwenye watoto 19 ana ujauzito mwingine wa mtoto wake wa 20 na anasema hana mpango wa kuacha kuendelea kuzaa katika siku za karibuni.
Martha, kutoka Medellin, Colombia, ana umri wa miaka 39 na anataka kuendelea kupata watoto hadi mwili wake utakaposhindwa kushika mimba tena.
Martha anasema anaona kuwa mama kwake ni kama biashara, na watoto wake wote amezaa na wanaume tofauti.
Martha anapokea msaada wa kifedha kutoka serikali ya colombia ambapo kwa mwezi anapokea takriban dollar 510 kwa ajili ya kuwatunza watoto wake wote.
"Nitaendelea kuzaa kwasababu kwangu inanilipa" alimalizia.