Anaweza akawa mtu mzee zaidi kuwahi kuapishwa kuwa Rais wa Marekani
Eric Buyanza
March 4, 2024
Share :
Joe Biden na Donald Trump, ambao huenda wakakabiliana katika uchaguzi ujao wa rais wa Marekani baadae mwaka huu, wote ni wazee. Lakini umri wao una jukumu gani katika kinyang'anyiro hicho, na wanaweza kuwavutia wapiga kura vijana?
Wakati chaguzi za mchujo kwenye vyama vyao ukiendelea, inaonekana kinyang'anyiro cha urais wa Marekani 2024 kitakuwa marudio ya 2020: Joe Biden dhidi ya Donald Trump. Hiyo ina maana kwamba siku ya uchaguzi, Novemba 5, 2024, wapiga kura wanaweza kuchagua kati ya mzee Trump mwenye umri wa miaka 78 Trump na Biden mwenye umri wa miaka 81. Iwapo hivyo ndivyo itakavyokuwa, mshindi atakaeapishwa Januari 20, 2025, atakuwa ndiye mtu mzee zaidi kuwahi kuapishwa kuwa rais wa Marekani.