pmbet

Anayehusishwa na Yanga kunasa kwenye rada za Zamalek.

Joyce Shedrack

May 27, 2025
Share :

Klabu ya Zamalek ya Nchini Misri inafikiria kumuajiri Kocha Rulani Mokwena wa Afrika Kusini kuwa kocha mkuu wa timu yao katika msimu ujao baada ya kocha huyo kuachana na Wydad Casablanca hivi karibuni.

Wydad star 'apologises' to Mokwena | Kickoff

Taarifa kutoka Misri zinaripoti bodi ya Zamalek imepitisha jina la kocha huyo huku baadhi ya viongozi wakisisitiza kuwa ni kocha mzuri licha ya kushindwa kupata mafanikio akiwa Nchini Morocco na kikosi cha Wydad.

 

Miongoni mwa orodha ya makocha wanaopewa vipaombele kukinoa kikosi cha Zamalek msimu ujao ni pamoja na Pitso Mosimane kocha wa zamani wa AL Ahly na Mamelodi Sundowns,Kocha wa zamani wa Esperance de Tunis raia wa Romania Laurentiu Reghecampf pamoja na Rulani Mokwena.

 

Ikumbukwe kuwa Zamalek inasaka kocha mpya wa kuifundisha klabu yao baada ya kuachana na Jose Peseiro kutokana na mfululizo mbovu wa matokeo kwenye ligi kuu Nchini humo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet