Anayemsumbua akili Perez Madrid huyu hapa
Sisti Herman
May 15, 2026
Share :

Wakati vuguvugu la kuelekea uchaguzi mkuu wa Real Madrid likikolea, wachezaji wa zamani wa timu hiyo Iker Casillas na Sergio Ramos wapo kwenye upande wa Timu ya mmoja kati ya wanaotajwa kuhitaji nafasi ya Florentino Perez, Enrique Riquelme ambapo Casillas, Sergio Ramos,Fernando Sanz, na Miguel Torres pia walihudhuria sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Riquelme mwezi Januari.
Enrique Riquelme alianza hatua zake za kwanza na wanachama wa klabu kwenye tukio lililofanyika Aprili 18, lililoandaliwa na Mtoto wa Fernando Sanz, rais wa zamani wa Madrid , pia alikuwepo kwenye tukio hilo.
Enrique Riquelme amekodisha eneo karibu na uwanja wa Santiago Bernabéu ili kufanya kampeni moja kwa moja kwenye lango la kuingilia uwanjani.





