pmbet

Anayetajwa kutua Simba alikuwa mchezaji bora kijana misimu miwili.

Joyce Shedrack

July 2, 2026
Share :

Aliyekuwa mchezaji wa timu za vijana za Nigeria Ibraheem Jabaar ameondoka Stellenbosch FC baada ya mkataba wake kumalizika, kufuatia pande zote mbili kushindwana kwenye maslahi akiwa anatajwa kutarajia kujiunga na Simba huku mashabiki wa timu yake wakiwa hawafurahishwi na uamuzi wa viongozi wake kushindwa kumbakiza nyota huyo.

Jabaar Set For Next Move After Stellies Exit - iDiski Times

Jabaar ameondoka Stellenbosch akiwa mmoja wa wachezaji walioacha alama kubwa katika historia ya klabu hiyo akishika nafasi ya nne kwa kucheza mechi nyingi zaidi akiwa na Stellenbosch, na ndiye mchezaji wa kigeni aliyeichezea klabu hiyo mechi nyingi zaidi, akicheza jumla ya mechi 140 katika mashindano yote ndani ya kipindi cha miaka mitano.

 

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 pia ameandika historia kwa kuwa mchezaji pekee kushinda tuzo ya Mchezaji Bora Kijana wa Msimu ya Stellenbosch mara mbili, baada ya kutwaa tuzo hiyo katika misimu ya 2021/22 na 2024/25.

 

Tetesi zinasema nyota huyo yupo karibu kumalizana na wekundu wa Msimbazi Simba ikiwa ni pendekezo la Kocha Steven Barker.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet