Anayetuhumiwa kifo cha Mandojo akamatwa na Polisi
Sisti Herman
August 13, 2024
Share :
Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma linamshikilia Raphael Keneth Ndamahnwa mlinzi wa kanisa Katoliki parokia ya watakatifu wote lililopo Nzuguni B kwa ajili ya uchunguzi wa kifo cha msanii wa muziki wa kizazi kipya Joseph Francis Maarufu kaka ManDojo kilochotokea agost 11 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi mwandamizi SACP Anania Amo ambaye amesema Jeshi Hilo linaendelea kumuhoji mtuhumiwa huyo kuhusiana na tukio hilo huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya uchunguzi zaidi